KWANINI UNASHINDWA KUFIKIRIA VITU VIKUBWA KWENYE MAISHA YAKO


 UTANGULIZI

        Ukweli ni kwamba ajionavyo mtu ndani mwake, ndio matokeo halisi ya maisha yake ya nnje. Ukisoma Maandiko ya Mungu kitab u cha Mithali 23:7; ‘Maana sonsvyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo...’ Hii na maana kwamba ukijiona mdogo ndani, basi hata mawazo yako hayawezi kuwa makubwa, maana hutegemea kile unacho kiona wewe ndani mwako, na sio watu wanavyokuona.

    Watu wengi hasa katika ukanda huu wa Afrika wameathiliwa sana na dhana ya ujumuishi, yaani mtu anajisemea au kujieleza katika makundi Fulani na kusahau kabisa kuhusu yeye mwenyewe. Utasikia mtu akisema sisi wakuria, familia yetu, sisi wanaume, au aaah hao ndio wahaya bwana.  Wewe ni mtu wa tofauti sana na wengine . Unaweza ukajiuliza sasa ni mambo gani hayo unayopasaswa kufanya ili kuondokana na hii hali ya kushindwa kufikia/ kupanga mambo makubwa kaaatika mipango ya mafanikio yako; endelea sehemu inayofuata hapo chini:-

-Ongeza ujuzi

-Amini kuwa unaweza

-Pata hamasa kutoka kwa watu waliofanikiwa

-Usiruhusu hali ya kukata tama

#1. Ongeza ujuzi

katika kile ambacho unakifanya hakikisha unakuwa masta. Katika hali ya kawaida ukiwa  unajua jambo Fulani vizuri sana; yani kila kitu kuhusu jambo hilo, huwezi kuwa mnyonge katika kulifanya/ kulisemea au kuliwekea mpango jambo hilo maana  unauhakika juu ya jambo hilo. Kwa mfano huwezi kuweka malengo ya kuwa daktari bingwa wa meno duniani na huku huna hata degree moja ya maswala ya utabibu. Ila ni kawaida daktari wa meno pale hospitali ya taifa muhimbili kuweka lengo la namna hii

#2. Amini kuwa unaweza

Katika kila jambo anza na wewe kwanza, amini katika uwezo wako binafsi ulionao katika kukammilisha jambo fulani. Usiamini katika watu wa nnje na kujisahau wewe mwenyewe ambae ndio mmiliki halali wa jambo hilo; kwa maana nyingine usitengeneze sababu za nnje za kufeli kwako, kwasababu utaanza kufikilia madhaifu walionayo nakukufanya wewe uanze kujipimia kiwango fulani kidogo cha malengo kuendana na uwezo wa watu hao

#3. Pata hamasa kutoka kwa watu walifanikiwa

Hakikisha unawafuata watu waliofanikiwa katika jambo ambalo wewe unataka kuwa; unaweza kuwafuata katika mitandao yao ya kijamii kama vile YouTube channels zao na Instagram akaunti zao, pale unaweza kupata taarifa mbali mbali ikiwemo makala za video na sauti ambazo unapaswa kusikiliza na zitakusaidia sana katika kukujenga na kukufanya uweze kukaa katika njia kuu kuelekea wazo lako ulilonalo. Kwamfano unawweza kuwafuata watu ambao ni mamenta kama vile Joel Nanauka na James Mwang’amba

Kwenye jambo hili hakikisha unapata hamasa za waatu hawa angalau kila siku ili iweze kukusaidia wewe kujenga imani ya nguvu za lengo hilo lilillopo ndani yako; itakufanya uweze kujiamini kuwa unaweza kufanya mambo makubwa.

#4. Usiruhusu hali ya kukata tamaa

Ukianza kifikilia tuu kwa habari ya uwezo ulionao nje kwa sasa basi unaanza kuruhusu hali ya kuvunjika moyo. Kumbuka kila kitu kinawezekana ukiamua, vitu kama vile elimu, kazi na familia vyote hivyo vinategemea wewe mwenyewe una mtazamo gani kuhusu mambo hayo yote. Mtazamo wa mtu ndio unaovutia fulsa mbalimbali katika maisha  yake; kwahiyo unapaswa kuwa na mitazamo chanya katika mambo yako ili kuepukana na hali ya kukata tama

Katika swala hili marafiki wanamchango mkubwa sana katika hali yako yakufanya mambo ukiwa na mtazamo chanya; jaribu kuwa na marafiki ambao sio kikwazo katika jambo unalolifanya kwa wakati huo. Mfano unakuwa na rafiki wa karibu ambae yeye haamini na hataki kufanya mazoezi ya viungo; kwa kawaida na wewe itakuwia ngumu kujihusisha na mambo hayo ya mazoezi hata kama ndio lengo lako kwa muda huo. Hapa naomba utambue aina na viwango vya urafiki

Hitimisho

Unapoamua kufanya jambo lolote lile kwenye maisha haya hakikisha unaaza na picha kubwa ya  jambo hilo. Usifiikilie kwa habari ya chanagamoto na uwezo wako wa sasa, kwa sababu kutoka katika picha kubwa unapaswa kulifanya /kuligawa jambo hilo katika visehemu vidogo vidogo ambavyo utaanza navyo; kwahiyo ni sawa na kusema kwamba unaweza ukala na kummaliza ng’ombe mzima endapo utamkata vipande vidogo vidogo, usijaribu mkumeza!

Sir, Seth

Sharing life experience, as others can learn from i.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

How do i meet HDI

Success from other people's opinions