Katika
safari yangu ya elimu miaka fulani nilipata bahati ya kwenda kusoma katika
shule moja huko kaskazini mwa nchi, na kama mwanafunzi mgeni katik
a shule ile
nilipata historia ya vitu vingi vizuri na vibaya ikiwemo taarifa za wakufunzi,
yaani waalimu wa shule ile. Moja kati ya taarifa za walimu ilikuwa ni hii
“Ohooh yaani huyu mwalimu wa bweni ni mnoko vya hatari kaa nae mbali, unaweza
ukaona kama anakuchekea kumbe ndo anakuchomea kule ofisini, kuwa makini” na
wanafunzi walikuwa wakimuogopa.
Baada
ya muda kidogo, tukawa na mahusiano mazuri tu na mwalimu mpaka nikawa naacha
vitu vyungu kwake, ikiwemo pesa begi
languo zisizo za shule na simu, ambavyo vitu hivyo ni haramu mwanafunzi kuwa
navyo shuleni. Na nikihitaji wakati wowote navipata hasa simu kwa aajili ya
mawasiliano. Uhusiano ulikuwa mzuri tu, na kwakuwa anaduka mtaani nikuwa
nachukua saa dukani kwake na kuja kuwauzia wanafunzi wenzangu pale shuleni. Na mpaka
nimemaliza nakuondoka mahusianao yapo vizuri kwamaana tuliendelea kuwasiliana
vizuri.
Katika
uhalisia wa maisha sehemu yoyote ile utakapoenda kwa mara yakwanza ni lazima
utakuwana na wenyeji watakao kupokea na kukupa maelezo na ABC za mazingira
hayo. Watu wengi katika kukueleza watasema mambo mengi ikiwemo kipi ni kizuri
chakufanya/kuchagua na kipi ni kubaya na hupaswi kufanya.
Kwa kawaida mtu huyo takueleza hisia zake juu ya
mambo au mtu fulani kutokana na mambo aliyoyapitia akiwa na mtu huyo. Kwa mfano
shuleni “mwalimu fulani kuwa nae mbali maana ni mtata sana” au kazini utasikia
“Kaa mbali na boss Kipara maana ni mnoko sana”. Sasa katika hali ya kawaida
wewe baada ya kuyasikia hayo yote ni lazima utatengeneza hali ya ‘tension’
unapokuwa katika miingiliano na hawa watu, kwasababu tayari ulishapandikizwa
chuki na ubaya wao.
Sasa
kimsingi, ni kweli hawa watu wanamabaya yao lakini hawakukufanyia wewe na
huwenda pia ni mabaya ya muda kitambo kilichopita, lakini usipokuwa makini
unajikuta na wewe unawachukia na kuwaona sio sahihi katika maisha yako, na
kuwafanya kuwa maadui zako. Sikiliza, kwa kufanya hivyo unajitengenezea mazingira
magumu katika safari ya kufanikiwa kwako, hapo kazini, shuleni, na sehemu
yoyote ambayo unapita.
Kuwa
na maadui ni kawaida katika maisha ya mwanadamu kwani inakupa namna ya kutatua
vikwazo katika safari ya kimaisha, lakini hakikisha ni adui uliomtengeneza wewe
mwenyewe, yaani chanzo cha uadui baina ya wewe na mtu mwingine kiwe na
mahusiano ya moja kwa moja kati yako na mtu huyo. Usikubali kutengenezewa
maadui.