Njia Ya Mafanikio
Katika Ulimwengu wa Utandawazi
“Usichokuwa
nacho jirani yako anacho fanya mawasiliano jibu lako lipo karibu yako tu.
Tatizo ni wewe umejifungia(Do not be Self-container to your development)” Stephin Fuime
Muda
mwingine sababu kuu ya kupitia hali ngumu ni wewe mwenyewe, kwasababu hutaki
kuzungumza na watu. Ukweli ni kwamba huyo jamaa ambaye wewe unamchukulia poa
ndie mwenye jibu la tatizo lako, pata muda wa kuwafahamu watu wanaokuzunguka;
yaweza kuwa majirani zako pale nyumbani, rafiki yako kule kazini, au watu katika
eneo lako la la mzunguzo wa kila siku: ni muhimu sana kuwajua watu.
Piga
picha kwamba wewe ni fundi gereji na una mteja wako ambae mara nyingi huwa
unamtengenezea gari lake, na mahusiano yenu yamebaki hapo tu, yaani unamjua
kuwa ni mteja wako pale kazini kwako (gereji) tu; hukutaka kujua zaidi kuhusu
mteja huyo. Na ukweli ni kwamba mteja wako ni wakili maarufu tu. Sasa siku moja
katika pilika pilika zako ukatakiwa passport ya kusafiria na katika mchakato wa
kuipata inakubidi uende kwa wakili ila kuapa kwa aajiri ya taarifa za wazazi
wako (affidavit). Swala hili lingekuwa rahisi sana kama ungekuwa unajua mteja
wako wa kila wakati kule kazini kuwa ni mwanasheria kwa maana ungemtafuta tu maramoja nae angefanya jambo, kwasababu
wewe ni mtu unaemfanyia vizuri akija kupata huduma ofisini kwako kule gereji.
Miaka
Fulani nilikuwa naishi makao makuu ya nchi, nilikuwa nimepanga chumba katika
nyumba moja kubwa iliokuwa na vyumba vingi, bahati nzuri kulikuwa na mfanyakazi
mwenzangu nayeye alikuja kupanga pale pale nilipokuwa nikiishi, maana ilikuwa
ni nyumba kumbwa tu yenye vyumba vingi vya kupanga. Basi siku moja nikiwa
natoka kazini jamaa angu alikuwa nyumbani siku hiyo hakwenda kazini, nikakutana
nae maeneo ya nyumbani nje pale, kwakuwa mimi nilikuwa nimechoka nikamwambia
jamaa angu kuwa vipi umepika jamaa akasema ana mawili apike au asipike maana
alikuwa ameshiba sana, basi mimi nkamwambia hakuna tatizo, basi mimi nikiwa na
uchovu wa kazi kutwa nzima niliingia ndani kwangu na kupika wali, wali
ulivyokuwa tayari kabla sijapika mboga
nikapakuwa kidogo nikala kwa kuwa nilikuwa na njaa sana, mara nikaongeza tena
na kujikuta nimeshiba tayari, hatimae nikajisemea mboga za nini tena natayari
nishashiba, nikaendelea na mambo mengine: ilikuwa ni mida ya saa 12 jioni.
Baadae
kidogo mida ya saa 3 usiku nikasema niende kumcheki jamaa ndani kwake, ghafla
nikamkuta jamaa hana chakula anakula mboga; yaani ana mboga hana chakula, na
mimi kule nilikula chakula bila mboga. Nikamwambia vipi kaka mbona unakula
mboga tupu, njoo uchukue chakula nimepika acha ujinga, kwakuwa nilimuuliza kuwa
kama atapika akasema hatapika, aliona haya na kusema “aah hamna shida bana
usijali”.
Kisingi
jamaa hakuwa na haja ya kulala na njaa kwa kula mboga pekee na mimi sikuwa na
haja ya kula chakula bila mboga, pale nilipomuuliza kuwa “utapika leo” angesema tuu kuwa mimi sina mpango wa
kupika ila ninamboga tayari ndani kama wewe utaweza pika chakula mboga zipo,
nakila mmoja wetu angekuwa mshindi
Katika
ulimwengu huu wa utandawazi usujaribu kufungia mawazo yako kwenye boksi kubwa
la ubinafsi, ongea na watu kwa sababu wataalamu wanasema, Ukitaka kufika nenda
mwenyewe ila ukitaka kufika mbali nenda na wenzako. Hii inamaanisha umoja
unanguvu zaidi kuliko kuwa pekeako katika kila jambo.
Wewe
kijana niwakati wako wa kutengeneza mtandao wa watu sasa, ukisoma kitabu
kinachoitwa His excellence the Head of
State kinasema “The matter is not what you know but who you know” sasa
kauli hiyo ikupe changamoto wewe, kwamba usiishie kujenga ujuzi tu, kwasababu ujuzi
pekee hautoshi; unahitaji kuwajua watu katika eneo lako la ujuzi.