IMANI ULIYONAYO CHANGANYA NA AKILI ZA UHALISIA WA MAISHA ULIONAYO ILI UWEZE KUWA NA FURAHA KATIKA MAISHA YAKO


           
Ukweli ni kwamba katika maisha yetu ya  kawaida kuna imani ambazo tunajengewa toka tukiwa wadogo, kwa malezi au hata katika dini zetu, mafunzo hayo na imani hizo kwa kiasi kikubwa ni nzuri na zenye kusaidia sana katika makuzi ya watoto katika jamii.

           Katika hali ya kaawaida kama mtoto akiyashika mafundisho na imani ya namna hii huwa na mwelekeo na tabia njema katika  maisha ya kwake. Lakini kwa manufaa na masilahi mapana ya maisha ya mtoto huyu kwa baadae anahitaji kuwa na maarifa makubwa sana ya kujiongeza ili asiweze kupoteza uhuru na furaha ya maisha yake anapokuwa mkubwa.

        Pamoja na kuwa na imani na mafunzo bora ya tabia njema katika jamii, mtoto huyu ambae kwa sasa ni mtu mzima anapaswa kuwa na mambo muhimu kadha wa kadha ili kuweza kuishi kwa amani na furaha katika jamii hii ambayo kwa kiasi kukubwa ina vitu na mapungufu mengi

# Kuendana na mazingira
# Kuwasaidia wengine
# Usijitenge na watu
# Kuwa makini katika yale unayoyafanya

#1. Endana na mazingira unayoishi

Ni kweli unafahamu kipi ni kizuri na kipi ni kibaya hiyo nifaida kwako, laikini sio kigezo cha kukufanya wewe uamue kuishi maisha yako tofauti kabisa na wenzio kama hauko katika dunia hii; hakika utakosa furaha ya maisha. Chukulia mfano wa mtu ambaye ana imani  kali juu ya maswala ya dini na kumjua mungu, sio vibaya kwa mtu kuwa hivi lakini ndo hata taarifa za kijamii huataki kuziskia katika maisha yako, kama vile taarifa, vipindi na makala mbalimbali katika redio na televisheni. Hiyo sio sahihi na utakosa furaha katika maisha maana hautakuwa wazi na mazingira ya dunia hii unayoishi ndani yake

#2. Kuwasaidia wengine

Tayari unfahamu mambo mengi kusuhu nidhamu, jinsi ya kuishi na watu vizuri na pengine hata dini unaijua vizuri tuu kwa imani yako, sasa vyote hivyo ukikaa navyo tu mwenyewe bado utakuwa hujafanya kitu katika maisha ya kwako. Ili kutimiza wajibu wako na deni ulilonalo unapaswa kuwasaidia wengine kwa namna moja au nyingine kwa kile ulichonacho ndani yako. Unaweza kuwasaidia kwa kuwaelekeza, kuwafundisha na kuwafanya wale unaoona kuwa wanakosea katika maadili ya maisha waige kutoka kwako, na sio kuishia kuwatenga na kusema watu fulani wanatabia mbaya nijitenge mbali nao. Hapana!

#3. Usijitenge na watu

Watu ni moja kati ya hazina kubwa katika kila mafanikio ya mtu, kwani ndiyo rasilimali kubwa katika kila uzalishaji. Katika maisha yakwako usijaribu kujiweka mbali na watu wanaokuzunguka kwa kuwatafsiri kutokana na tabia au myenendo yao katika jamii, wafanye wawe watu wako na wewe uwe chachu ya mabadiliko yao katika maisha. 

#4. Kuwa makini katika yale unayoyafanya

Unapokuwa mtu mwenye kila sababu ya kusema kuwa unanidhamu, unaishi katika imani na unataka kuwa na maisha yenye furaha, unapaswa kuwa makini katika yale unayoyafanya ili kutimiza kusudi lako. Muda mwingine unaweza kujihusisha na makundi ambayo katika jamii yanadharauliwa, kusemwa vibaya na kuchukuliwa watu wasio haki katika jamii, hivyo unapaswa kuwa makini pia namna jinsi ya kuchanganyika nao kwa mfano; walevi, wavuta bangi, malaya na makundi mengine maovu katika jamii

             Lengo kuu la makala hii ni kukufanya wewe unaejiona kuwa uko sawa katika maisha, katika tabia, imani ya dini  na nidhamu, usiishie tu kujihesabia haki katika maisha yako na kusema kuwa wewe sio kama wengine,  bali kuwa baraka kwa wengine katika jamii na watu kufaidika na kile ulicho kuwa nacho ndani yako. Na haina maana kudharau na kuona kile ulichonacho hakifai na hakina maana yoyote, hapana wewe ni bora na mtu muhimu sana katika jamii.


Sir, Seth

Sharing life experience, as others can learn from i.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

How do i meet HDI

Success from other people's opinions